Gordon Brown amesema katika mahojiano ya leo na gazeti la Guardian kwamba: "Muda mdogo sana umesalia ili kuzuia mdororo wa kiuchumi unaoweza kuepukika." Gordon Brown ameashiria kuongezeka vita vya kibiashara, utozaji ushuru mkubwa, vizuizi vya uwekezaji na uwezekano wa kukabiliana nchi zenye uchumi mkubwa duniani katika vita vya sarafu na kusisitiza kuwa mamilioni ya ajira yako hatarini.
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza ametahadharisha kuwa japokuwa viongozi wa Marekani wamezungumzia kuongezeka mivutano mkabala wa sera za ushuru za Trump lakini lengo la mwisho la Trump ni kurejesha uzalishaji nchini Marekani.
Amesema, kusitisha kwa siku 90 baadhi ya ushuru sio ishara yoyote ya kupunguza hali ya mivutano.
Brown ameashiria tajiriba ya mgogoro wa fedha wa mwaka 2008 na kusisitiza kuwa kupatiwa ufumbuzi migogoro mbalimbali inayoikabili dunia kunahitaji majibu ya kimataifa na yaliyoratibiwa. Amependekeza kuasisiwa "muungano wa kiuchumi wa nchi zenye mwelekeo mmoja" ili kukabiliana na mdororo wa kiuchumi duniani, sawa na muungano ulioundwa kusaidia Ukraine.
342/
Your Comment